Vitengo vya Ofisi

Majukumu ya Kitengo cha Kaguzi za Mikoa
  • Kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara wa Skuli na mwalimu mmoja mmoja kama ilivyofafanuliwa katika Mfumo wa Ukaguzi uliowekwa na Ofisi.
  • Kuhakikisha kuwa mtaala uliokubalika ndio unaotumika kwa ajili ya kuleta ufanisi wa utoaji wa elimu katika skuli.
  • Kuweka Viwango vya Ukaguzi na viashiria vya utekelezaji ili kudumisha ubora wa Skuli katika masuala ya uongozi na uendeshaji, ufundishaji na ujifunzaji, msaada kwa wanafunzi na matokeo ya kujifunza.
  • Kushajihisha matumizi ya teknolojia ya habari na mawasilino kwa lengo la kuongeza ufanisi katika ukaguzi wa elimu.
  • Kuzielekeza skuli zilizokaguliwa juu ya mambo yanayohusu uimarishaji wa elimu bora kwa kuzingatia taarifa za utendaji wa skuli na ripoti za ukaguzi.
  • Kutoa Ripoti ya kila mwaka ya ukaguzi wa elimu na kutoa mrejesho wa uthibiti ubora kwa wadau wa elimu.
Majukumu ya Kitengo Uhasibu
  • Kuandaa na kufanya malipo mbalimbali ya Ofisi
  • Kuandaa taarifa za mapato na matumizi kwa kila mwezi, robo mwaka, nusu na mwaka kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Fedha.
  • Kutayarisha hati za malipo kwa watumiaji kwa mujibu wa kasma za mgao wa Ofisi.
  • Kuandaa malipo na kuyawasilisha katika mifuko na makato maalum ya watumishi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zinazohusika.
  • Kufuatilia upatikanaji wa fedha zilizotengwa.
  • Kufanya usuluhisho wa hesabu za Ofisi (Bank Reconciliation).
Majukumu ya Kitengo Cha Manunuzi
  • Kuandaa na kutekeleza mpango wa ununuzi wa mwaka wa Ofisi na kuandaa taarifa ya utekelezaji wake.
  • Kufanya tathmini ya uchakavu wa vifaa na samani za Ofisi, kuamua mwisho wa matumizi yake na kuvifuta kwenye daftari la mali za Ofisi.
  • Kuandaa daftari la mali za Ofisi.
  • Kuandaa mapendekezo ya bajeti ya kitengo ya kila mwaka
  • Kuandaa zabuni na kuratibu usimamizi wa utekelezaji wake.
  • Kununua, kutunza na kusimamia usambazaji wa vifaa na huduma mbalimbali za Ofisi kwa mujibu wa Sheria na Miongozo ya Ununuzi.
Majukumu ya Kitengo cha Sheria
  • Kutoa ushauri juu ya masuala yote ya kisheria na kusaidia katika kutoa tafsiri juu ya sheria na mikataba mbalimbali kwa Ofisi ili kuliwezesha kutekeleza majukumu yake.
  • Kushiriki na kutoa ushauri wa kisheria wakati wa majadiliano mbalimbali yanayohusu Mamlaka juu ya makubaliano au mikataba maalumu.
  • Kuandaa mapendekezo ya bajeti ya kitengo ya kila mwaka.
  • Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sheria na taratibu mbalimbali katika Ofisi na kutoa ushauri ili kuziboresha zaidi
  • Kushirikiana na Mwanasheria Mkuu katika kushtaki na kuendesha kesi za madai.
  • Kuandaa nyaraka mbali mbali za kisheria
Majukumu ya Kitengo cha TEHAMA
  • Kushauri juu ya mambo yanayohusiana na teknolojia ya habari na mawasiliano.
  • Kutayarisha na kusimamia tovuti ya Ofisi.
  • Kuhifadhi na kusimamia kumbukumbu, taarifa na nyaraka zote zilizomo katika hati laini (soft copies)..
  • Kuandaa na kusimamia data base ya Ofisi
  • Kuandaa na kutekeleza mkakati wa mawasiliano wa Ofisi.
  • Kuratibu uandaaji wa taarifa na nyaraka mbalimbali za Ofisi kusambaza nyaraka, vipeperushi, vitabu na taarifa za kielektroniki