Idara za Ofisi
Idara ya Rasilimali Watu Mipango na Utawala
Idara ya Rasilimali Watu, Mipango na Utawala ni idara muhimu kinachohusika na usimamizi wa masuala ya rasilimali watu, upangaji wa mikakati, na utoaji wa huduma za utawala katika taasisi..
- 1 Kutoa huduma za kiutawala na uendeshaji
- 2 Kushughulikia masuala mbalimbali ya rasilimali watu kama vile mafunzo, upimaji utendaji kazi, mkataba wa utoaji wa huduma, mishahara na stahiki nyengine za watumishi nk
- 3 Kuratibu uandaaji, utekelezaji na kufanya ufuatiliaji na tathmini za kazi za Ofisi
- 4 Kutoa mwongozo na utaalamu wakati wa uandaaji wa mipango, viashiria vya utekelezaji (Key Performance Indicators) pamoja na taarifa za utekelezaji wa kazi za Ofisi
- 5 Kuandaa mfumo na muundo wa ukusanyaji wa taarifa na ripoti za utekelezaji
- 6 Kukusanya taarifa mbalimbali, kufanya uchambuzi, na kutambua masuala mbalimbali yanayopaswa kujumuishwa katika takwimu za Ofisi
Idara ya Viwango na Uthibiti Ubora wa Elimu
Idara ya Viwango na Uthibiti Ubora wa Elimu inahakikisha kuwa viwango vya elimu vinazingatiwa katika taasisi zote za elimu kwa mujibu wa sera, sheria, na miongozo ya serikali
- 1 Kuratibu shughuli zote za ukaguzi.
- 2 Kuhakikisha kuwa ukaguzi unafanyika kwa mujibu wa mitaala iliyokubalika
- 3 Kuandaa ripoti ya ukaguzi ya robo na mwaka na kuiwasilisha kwa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu
- 4 Kuhakikisha kuwa ukaguzi wa elimu unafanywa kwa mujibu wa Mfumo uliokubaliwa na Ofisi.
- 5 Kuweka viwango vya ukaguzi na viashiria vya utekelezaji ili kudumisha ubora wa ukaguzi
- 6 Kushajihisha matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa lengo la kuongeza ufanisi katika ukaguzi wa elimu
- 7 Kuandaa mikakati ya uimarishaji wa ubora wa elimu inayotolewa.
Divisheni za Idara
- 1 Divisheni ya Risilimali Watu
- 2 Divisheni ya Utawala
- 3 Divisheni ya Mipango
- 4 Divisheni ya Utunzaji Kumbukumbu
Divisheni za Idara
- 1 Divisheni ya Viwango na Uthibiti Ubora wa Elimu
- 2 Divisheni ya Utafiti