Mkaguzi Mkuu wa Elimu
Karibu kwenye tovuti yetu rasmi! Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu Zanzibar inajivunia kuwa sehemu muhimu ya kuimarisha mfumo wa Elimu kwa kuhakikisha ubora wa Ufundishaji na Ujifunzaji katika Skuli zetu.
Tunatambua kuwa elimu ni msingi wa maendeleo ya jamii yoyote, kwa pamoja tuna jukumu la kuhakikisha kuwa tunaimarisha viwango vya elimu kwa kufuata sera, sheria, na miongozo iliyowekwa.
Napenda kuwahimiza Viongozi wa Skuli, Walimu ,Wazazi na wadau wote wa elimu kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yetu kwa bidii, weledi, na uadilifu ili kufanikisha lengo kuu la kuwa na elimu bora kwa kila mwanafunzi.
Kupitia usimamizi mzuri na juhudi za pamoja, tunaweza kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya elimu na kusaidia kujenga kizazi chenye maarifa, ujuzi, na maadili mema kwa maendeleo ya taifa.
Ahsanteni kwa kutembelea tovuti yetu. Tushirikiane kwa dhati katika kuinua elimu kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.