Majukumu ya Ofisi

  • Kufanya Ukaguzi wa mara kwa mara wa skuli na mwalimu mmoja mmoja kama ilivyofafanuliwa katika Mfumo wa Ukaguzi uliowekwa na Ofisi.
  • Kuhakikisha kuwa mataala uliokubalika ndio unaotumika kwa ajili ya kuleta ufanisi wa utoaji wa elimu katika skuli.
  • Kuweka viwango vya ukaguzi na viashiria vya utekelezaji ili kudumisha ubora wa skuli katika masuala ya uongozi na uendeshaji, ufundishaji na ujifunzaji, msaada kwa wanafunzi na matokeo ya kujifunza.
  • Kufanya ukaguzi wa elimu kwa skuli inayopendekezwa kuanzishwa kabla ya kuanzishwa na kusajiliwa, na kutoa mapendekezo na ushauri kwa mamlaka zinazohusika.
  • Kushauri kuhusiana na utendaji wa walimu wakuu na walimu katika kutekeleza majukumu yao katika skuli kama yalivyoelekezwa katika viwango vya taaluma ya ualimu na maadili, miongozo ya wizara na kanuni za ukaguzi.
  • Kushajihisha matumizi ya teknolojia ya habari na mawasilino kwa lengo la kuongeza ufanisi katika ukaguzi wa elimu.
  • Skuli zilizokaguliwa juu ya mambo yanayohusu uimarishaji wa elimu bora kwa kuzingatia taarifa za utendaji wa skuli na ripoti za ukaguzi.
  • Kutoa ripoti ya kila mwaka ya ukaguzi wa elimu na kutoa mrejesho wa uthibiti ubora kwa wadau wa elimu.
  • Kufanya utafiti kwa kuzingatia mambo yaliyobainika katika ripoti za ukaguzi wa elimu.
  • Kutekeleza kazi nyengine yoyote inayohusiana na ukaguzi kama itakavyoelekezwa na Waziri.