Profile Photo
Nd.Maimuna Fadhil Abass
Mkaguzi Mkuu wa Elimu-Zanzibar

Nina furaha kubwa na shukrani
kuwakaribisha kwenye tovuti yetu.
Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu Zanzibar
(OCIE)

Kuhusu Taasisi

Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu Zanzibar ni Taasisi ya Serikali chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar iliyoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Kuanzisha Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu Namb. 10 ya mwaka 2018. Ofisi hii hutumia ufupisho wa Kiengereza OCIE (The Office of Chief Inspector of Education).
Awali ilikuwa Idara ya Ukaguzi wa Elimu Zanzibar. Ili kukidhi vyema dhima ya Ofisi hii, ilibadilishwa kutoka Idara ya Ukaguzi na kuwa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu Zanzibar mwaka 2011.
Ofisi hii imeanzishwa kwa malengo ya kuhakikisha kuwa elimu inatolewa kwa mujibu wa sera, sheria na miongozo ya Serikali na taasisi zinafundisha kwa mujibu wa mitaala iliyoidhinishwa kwa ngazi husika. Vile vile kuhakikisha kuwa miiko na maadili ya kazi ya Ualimu inafuatwa, kushauri juu ya viwango bora vya uendeshaji wa skuli, ufundishaji na ujifunzaji, kuwasaidia wanafunzi pamoja na kutumia zana sahihi za upimaji.

Matangazo

  • MAR 17 2026

    Mafunzo ya Wakaguzi wa Wapya kuhusu Muongozo wa Ukaguzi

    Kiembe Samaki TC

Ukaguzi wa Skuli

Regulatory

kuangalia mazingira salama, mtaala unaofaa kwa watoto wadogo, na mbinu shirikishi za ufundishaji.ili kuhakikisha msingi mzuri wa kusoma, kuandika, na kuhesabu

Ngazi ya Maandalizi
Quality Assurance

Utekelezaji wa mtaala, ushiriki wa wanafunzi, uwiano wa walimu kwa wanafunzi, na upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia ili kuhakikisha watoto wanapata maarifa yatakayowasaidia.

Ngazi ya Msingi
Advisory

Ubora wa ufundishaji, ufanisi wa walimu, matumizi ya teknolojia, na usimamizi wa nidhamu kwa maandalizi ya elimu ya juu pamoja na soko la ajira

Ngazi ya Sekondari

Habari na Matukio

8 March 2026

Afisi ya Elimu Wilaya Mjini, Zanzibar

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mkaguzi Mkuu wa Elimu Zanzibar Washiriki Kikao cha Kupitia Muongozo wa Ukaguzi wa Vyuo wa Ualimu . ...

Soma zaidi

13 March 2026

Kiembe Samaki TC, Zanzibar

Wakaguzi Wapya Wapatiwa Mafunzo ya Ukaguzi juu Miongozo ya Ukaguzi ...

Soma zaidi

8 December 2025

Ofisi ya Mkaguzi wa Elimu, Vuga Zanzibar

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Mhe.Hussein Ali Suleiman akitoa Maelezo ya Ofisi Wakati wa Ziara ya Ukaribisho wa Waziri wa Elimu.

Soma zaidi